Ni taarifa ambazo zimechukua headlines usiku wa July 12 baada ya watu wanaosadikiwa kuvamia kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga Dar na kuuwa watu saba.
Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi (IGP), Ernest Mangu…’Nasikitika kuwapa taarifa kuwa majambazi walivamia kituo cha polisi cha stakishari na kupiga risasi na kuua Askari polisi wanne na raia watatu. Majambazi hao walikuja kama raia wakawaida wanaohitaji huduma walipofika kituoni na kuulizwa shida yao nini ndipo walipoanza kuwashambulia askari walio kuwa kituoni
Raia waliouwawa ni raia ambao walikuwa wamekuja kituoni kutoa taarifa za matukio ya kwao ya kawaida wapo pia askari ambao wamejeruhiwa na raia waliojeruhiwa wapo hospitali wanapata matibabu
Nikweli kuna silaha ambazo zimeporwa miongoni ni zile ambazo za askari ambao walikuwa ulinzi hapa na zingine zilikuwa chumba cha mashitaka.uchunguzi unaendelea kujua silaha ngapi zimeporwa wakati tukipata taarifa mpya tutazitoa
Tukio hilo la kusikitisha lazima sheria ichukue mkondo wake kuwapata hao waliohusika na tukio hilo.kama mnakumbuka tukio kama hili lilitokea Ushirombo walivamia kituo kama hiki walisababisha mauaji kwa Askari sisi hatutachoka tutahakikisha tunapambana nao mpaka tunawapata
Nibaadhi ya silaha ambozo zilihusika katika mapambano kati ya polisi na majambazi katika kituo cha polisi
Picha na Abduly Makuka jr
No comments:
Post a Comment