suppot

Wednesday, 15 July 2015

MAPOKEZI YA DK. MAGUFULI YATIGISHA DAR, WANANCHI KWA MAELFU WAFURIKA VIWANJA VYA ZAKHEM, MBAGALA KUMSHUHUDIA


Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam akimpokea Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji hilo.



Dk. Magufuli akizungumza wakati wa mapokezi yake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofika kumshuhudia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli kwenye Viwanja vya Zakhem, Mbagala Dar es Salaam, 


Wakazi wa Mbagala wakiwa wamejipanga barabarani kumuona mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli

Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nnauye akiwasili kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala akiwa kwenye usafiri wa Boda boda.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.


Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mbagala Zakheem tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa Dar es Salaam.


Dk. John Pombe Magufuli mgombea wa Urais kupitia CCM akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Idd Azzan wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano Zakheem Mbagala.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Dar es Salaam.






Mgobea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakizicharaza tumba, kusaidia wakati bendi ya TOT Plus ilipokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi ya mgombea huyo kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo

Picha na (Makuka jr)

No comments:

Post a Comment