suppot

Tuesday, 21 July 2015

wiz kid ft Drake ojuelegba (remex)

UANDIKISHAJI WA KUPIGA KURA KWA UCHAGUZI WA URAIS KWA MASHINE ZA BVR









                 




                                 Baadhi ya mashine za uandikishaji wa kupiga kura BVR

Mgombea wa urais wa Chadema akijiandikisha kupiga kura

Baadhi ya wananchi wakijiandikisha kupiga kura kwa kutumia mashine za BVR

Friday, 17 July 2015

BREAKING NEWZ!!!!! MWANAMUZIKI WA DANCE BANZA STONE AFARIKI



Muimbaji wa muziki wa dansi aliyewahi kutamba akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta na TOT Band, Ramadhan Masanja maarufu kama Banza Stone amefariki dunia mchana wa Ijumaa, July 17.
  

Banza alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Taarifa kuhusu kifo chake zimethibitishwa na kaka yake pamoja na mmiliki wa Twanga Pepeta, Asha Baraka. 
  
Kwa mujibu wa kaka yake, Jabir Masanja, msanii huyo alikuwa anasumbuliwa na fangasi kichwani mwake na dawa alizokuwa anatumia zilikuwa kali kiasi cha kumpotezea hamu ya kula.
  
Hivi karibuni mama yake mzazi aliongea na kituo cha redio cha EFM na kukiambia kuwa afya ya mwanae ilizidi kuzorota na alianza kugoma kula chakula wala kunywa kunywa dawa. Mama huyo alisema hadi siku hiyo Banza alikuwa amegoma kula kwa siku tatu mfululizo. 
  
Aliongeza kuwa pamoja na kuugua hivyo bado wasanii wenzake walishindwa kwenda kumjulia hali.
  
“Mpaka sasa sijamuona mtu yeyote aliyekuja kumshughulikia na kumwangalia, wamemwacha hivi hivi. Na mimi siwezi kuwalaumu kwanini hamjaja kumwangalia, kila mtu na moyo wake, mwenye kuja atakuja, mimi ntahangaika na mtoto wangu mpaka pale atakapoamua mwenyezi Mungu,” alisema Mama Banza.
  
Kabla ya hapo muimbaji huyo alizushiwa kufariki mara nyingi. Wiki chache zilizopita Banza alimongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM kukanusha.
  
“Ndio naumwa kichwa kina nisumbua sana lakini sasa hivi naendelea vizuri yaani hizo habari za kuzushiwa kifo naona sasa hivi kwangu sijui hata itakuwa mara ya ngapi, maana nimeshazushiwa sana. Mimi mzima na huyo anayeeneza azunguke na mikoa mingine aeneze vizuri,” alisema Banza.
  
“Lakini mimi nipo nyumbani hapa Sinza kwa Mama yangu sasa hivi hapa napata juice yaani marehumu anaongea,” aliongeza Banza kwa kicheko.
  
“Inshallah nikiwa vizuri mashabiki wangu wataniona tu lakini nipo mzima.”
  
Msiba upo nyumbani kwao Sinza, Dar es Salaam. Kwa wale wanaopenda kuchangia msiba wake wanaweza kumchangia kwa kutumia namba: 0715407088 au 0753786016.
  
Mungu ailaze mahali pema peponi. Amen.


Makuka jr(Admin)

EID! EID! EID! BLOG YETU INAWATAKIA SKUKUU NJEMAA


TUNAWATAKIA SKUKUU NJEMA KESHOO

Makuka jr(admin)

Wednesday, 15 July 2015

MAPOKEZI YA DK. MAGUFULI YATIGISHA DAR, WANANCHI KWA MAELFU WAFURIKA VIWANJA VYA ZAKHEM, MBAGALA KUMSHUHUDIA


Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam akimpokea Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji hilo.



Dk. Magufuli akizungumza wakati wa mapokezi yake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofika kumshuhudia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli kwenye Viwanja vya Zakhem, Mbagala Dar es Salaam, 


Wakazi wa Mbagala wakiwa wamejipanga barabarani kumuona mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli

Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nnauye akiwasili kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala akiwa kwenye usafiri wa Boda boda.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.


Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mbagala Zakheem tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa Dar es Salaam.


Dk. John Pombe Magufuli mgombea wa Urais kupitia CCM akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Idd Azzan wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano Zakheem Mbagala.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Dar es Salaam.






Mgobea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakizicharaza tumba, kusaidia wakati bendi ya TOT Plus ilipokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi ya mgombea huyo kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo

Picha na (Makuka jr)

Tuesday, 14 July 2015

UVAMIZI WA KITUO CHA POLISI CHA STAKISHARI


Ni taarifa ambazo zimechukua headlines usiku wa July 12 baada ya watu wanaosadikiwa kuvamia kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga Dar na kuuwa watu saba.

Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi (IGP), Ernest Mangu…’Nasikitika kuwapa taarifa kuwa majambazi walivamia kituo cha polisi cha stakishari na kupiga risasi na kuua Askari polisi wanne na raia watatu. Majambazi hao walikuja kama raia wakawaida  wanaohitaji huduma walipofika kituoni na kuulizwa shida yao nini ndipo walipoanza kuwashambulia askari walio kuwa kituoni



Raia waliouwawa ni raia ambao walikuwa wamekuja kituoni kutoa taarifa za matukio ya kwao ya kawaida wapo pia askari ambao wamejeruhiwa na raia waliojeruhiwa wapo hospitali wanapata matibabu
 
Nikweli kuna silaha ambazo zimeporwa miongoni ni zile ambazo za askari ambao walikuwa ulinzi hapa na zingine zilikuwa chumba cha mashitaka.uchunguzi unaendelea kujua silaha ngapi zimeporwa wakati tukipata taarifa mpya tutazitoa 


Tukio hilo la kusikitisha lazima sheria ichukue mkondo wake kuwapata  hao waliohusika na tukio hilo.kama mnakumbuka tukio kama hili lilitokea Ushirombo walivamia kituo kama hiki walisababisha mauaji kwa Askari sisi hatutachoka tutahakikisha tunapambana nao mpaka tunawapata


Nibaadhi ya silaha ambozo zilihusika katika mapambano kati ya polisi na majambazi katika kituo cha polisi 

Picha na Abduly Makuka jr

Tuesday, 5 May 2015

Mgomo wa Madereva wasababisha vurugu mbagala



              Baadhi ya wakazi wa Mbagala wakizuia barabara kutokana mgomo wa madereva
(picha na makuka jr)

Mayweather amchapa Paquiao

 Hatimaye bondia FLOYDE MAYWEATHER aibuka kidedea kwa kushinda pambano dhidi ya PAQUIAO na kutwaa ubingwa wa WFB,HBO,PBO kwa points


Ushahidi wa Majaji wa Mpambano huo wakionesha matokeo ya mchezo huo ingawa watu wanasema kuwa FLOYDE MAYWEATHER hakushinda kihalali.
(picha na Makuka jr)

Rekodi za mabondia kati ya Paquiao na Mayweather


Ni baadhi ya rekodi za mabondia hao. je? Nani ataibuka kidedea na kuweka historia ya Dunia usikose kufatilia blog yetu ya harakati za Mtaa kwa taarifa muhimu zaidi

Mpambano mkali wa Dunia

Ule mpambano wa masubwi wa Dunia kati ya Bondia wa Philpino Manny Pacquiao na Marekani Floyde Mayweather umekaribi ambapo leo mabondiaa hao wamepima uzito na kutambiana

Saturday, 28 March 2015

MWANZILISHI WA TIP TOP CONNECTION ABDU BONGE AFARIKI DUNIA

                Aliyekuwa meneja na Mwanzilishi wa Tip top connection ABDU BONGE amefariki
                                                             dunia jana mach 28.

                      Kwa Mujibu wa chanzo chetu cha habari Abdu Bonge alikuwa akiugua


             Harakati za mtaa blog Chini ya DOP Dully zinatoa pole kwa familia ya Bonge na Wafiwa
                          wote mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amin
                               Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

                                                         Tutawaletea Habari Zaidi

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA AFRIKA NA CHINA,RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA


Mgeni rasmi wa Kongamano la tatu la Viongozi vijana wa Afrika na China,Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akihutubia usiku wa jana kwenye kongamano hilo lililo fanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ngurdoto Arusha



Katibu mkuu wa CCM, Ndugu Abraham Kinana akizungumza katika kongamano hilo mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

Rais kikwete akitoa salamu zake kwa washiriki wa kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,Ambalo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Zimbabwe

Rais Jakaya kikwete akipewa tuzo ya heshima juu ya kuhamasisha Amni na utulivu Barani Afrika na Rais wa Umoja wa Vijana Afrika
(PAYU) Francine Furaha Muyumba.Tuzo hiyo imetolewa na umoja wa Vijana wa Afrika,pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi 
Mh. Mboni Mhita

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la umoja wa viongozi vijana wa Afrika na China,Ambapo Mgeni rasmi alikua ni Rais wa Zimbabwe 
Mh. Robert Mugabe

Rais Kikwete akizungumza jambo na katibu mkuu wa CCM ndug Kinana alipo wasili jioni ya jana 
katika moja ya ukumbi wa mikutano  hoteli ya Ngurdoto mjini Arusha, kwa ajili ya kutoa salamu kwa washiriki wa kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China
Ambalo mgeni Rasmi alikua ni Raiswa Zimbabwe ,Robert Mugabe
Pichani kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais -Mazingira Mh. Stephan Masele.
Picha zote na (DOP Abduly Makuka)


Kushoto bondia wa kichina kimso lee akitamiana na bondia wa kitanzania baja  ili kuoneshana ubavu ijumaa kweny pambano la utangulizi kati ya Kaseba na Maugo.
@.picha na Abduly makuka
Mabondia Japhet kaseba kushoto akitunisha misuli na Mada maugo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wa jana Ijumaa katika ukumbi wa Diamond jublee

Friday, 27 March 2015

Pasaka! Pasaka ! Pasaka!

IT'S ALL ABOUT MUSIC 
Chiwileinc Entertainment inakudondoshea show la kibaba likihusisha Amir mill, Fraga de Pro Sam Flavour Mwailonda Masia, Y-sam, Claver B, Masai wa kigoma Nzasa Hood & Dienova, siku ya Pasaka katika ukumbi wa Manchester Pub mbagala dar es salaam kwa kiingilio cha #3000 wanaume wakati wadada watachangia #2000 tu hii ndio nafasi kuja kucheza nikupeti peti na Dunia mzima Live Bila kusahau mixng kali toka kwa ma Dj DOP Kukaa

MSAKO MKALI

Waganga wa Jadi Wawapinga Mkwara Jeshi la Polisi, Wasema Tabia ya Kufanya Msako na Kuchukua Vibuyu vya Itawatokea Puani 
Wakati msako wa kuwakamata waganga wapiga ramli chonganishi ukiendelea nchi nzima CHEKI HAPA=>http://bit.ly/1zZzENW hasa katika mikoa ya kanda ziwa, jeshi la polisi nchini limepewa onyo toka kwa wanganga wa jadi juu ya vifaa vinavyokamatwa wakati wa msako wao.CHEKI HAPA=>http://bitly.com/1MBFSf4